Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Wapiganaji wa kundi la kigaidi la Daesh wamewauwa kiasi cha magaidi 25 wa makundi mengine yanayolenga kuiangusha serikali ya Syria katika shambulio lililofanywa usiku ndani ya eneo lililowekwa na Uturuki na Marekani kuwa lisilokuwa na shughuli za kijeshi ikiwa ni mbinu wanazodai kuwa ni za kupambana na kundi hilo la kigaidi lenye itikadi kali.
Shambulio hilo la magari manne ya mabomu lilifanyika karibu na mji wa Marea, sehemu muhimu katika ukanda huo salama unaounganisha magaidi katika mji uliogawika wa Aleppo na njia zao za kuwapatia mahitaji kuelekea katika mpaka na Uturuki.
Shambulio hilo limekuja huku kukiwa na ishara kwamba hatua za kuunda eneo hilo salama katika maeneo ya jimbo la Aleppo ambalo kwa sasa linadhibitiwa na magaidi wa Daesh ambao walikuwa wakipata mafunzo na misaada kutoka Uturuki zinapata kasi.
Kundi kubwa la magaidi nchini Syria , Ahrar al-Sham, leo limekaribisha rasmi mpango huo wa Marekani na Uturuki wa kutaka kuiangusha serikali halali ya Syria, likisema ni kwa maslahi ya watu wa Syria pamoja na usalama wa Uturuki.
Mwisho wa habari/ 291